Saturday, October 14, 2017

SAFARI YA MJASIRIAMALI,

Je, kwa nini hakuna mitaji kwa vijana wengi?
katika dunia tunayo ishi leo idadi ya vijana ni kubwa sana hasa katika nchi ya ulimwengu wa tatu na wa pili yaani nchi maskini na zile zenye uchumi unaokua kwa kasi. idadi hii kubwa ni nguvu kazi kwa maana ya rasilimali watu katika uzalishaji, uongozi na nyanja zote za maisha ya kawaida.

Vijana wetu wanakosa mitaji kwa kuwa hawana mambo makuu manne muhimu sana katika uchumi kama yafuatayo,
  1.   Ujuzi na usimamizi dhabiti wa rasilimali (yaani managerial competency) kijana anapokuwa na uelewa wakina juu ya mambo ya utawala wa rasilimali zilizopo utafanikiwa kupata fursa nyingi na kwa namna rahisi sana ili kuleta tija katika jamii anayoishi. Hii ina ambatana na ubunifu wa kujua ujuzi alionao kijana, kipaji, fursa watu iliyo mzunguka kama msemo usemao "maisha ni watu" watu ni wateja wa bidhaa na huduma mbalimbali.
  2.  Ujuzi na uwezo wa kapanga  mipango thabiti inayotekelezeka kwa uwezo wake mwenyewe (yaani proper planning and sustainable strategies). kijana wa karne hii lazima awe na uwezo mkubwa wa kuona mbali katika mawazo aliyonayo na kuyaweka kimkakati ili aweze kuleta maendeleo endelevu katika maisha ya kila siku na jamii yake. asipokuwa mbunifu katika mpangilio wa mipango yake itakuwa ngumu hata yeye kujua nini anahitaji kwa kiasi gani na lini kwa namna gani.
  3. Ujuzi na maarifa ya fedha (yaani financial intelligence) kijana akiwa na ujuzi mali na maarifa ya fedha ni rahisi kuelewa wapi anaweza kupata fedha bila kusahau mambo mengine hapo awali ilikupata pesa ya kuendesha miradi yake kwa mfano tanzania inatoa 5% ya mapato yake kuwezesha vijana has walio rasimisha miradi yako na wenye andika nzuri la miradi katika kila halmashauri nchini, kuna mashirika marafiki wa uchumi na maendeleo yanayotoa huduma pia. mtu mwenye ujuzi wa pesa halalamiki ugumu wa fedha ila unahitaji sera nzuri za uwekezaji na mazingira ya biashara na kulipata kodi stahiki.
  4. Mwisho ni Elimu na ujuzi wa uwekezaji (yaani Investment knowledge and skills) kijana mwenye kujua fursa na utaratibu wa uwekezaji ni rahisi kuamini uwezo wake wa kuleta mawazo yake kwenye mazingira ya uwekezaji kwa kufahamu fursa nyingi (incentive opportunities) katika baadhi ya sector na ushindini wa kimasoko katika mahali husika.

0 comments: