Friday, October 20, 2017

MRADI MKUBWA WA URANIUM WA MTO MKUJU NI MKUBWA SANA DUNIANI Tanzania ya anza kunifaika na Madini yaliyopo Nchini.


Tanzania inatarajiwa kuwa nchi kubwa tano kwa uzalishaji wa madini ya Uranium Afrika baada ya kukamilika kwa mradi wa Uranium wa Mto Mkuju. Mradi huu ulianza miaka 7 iliyopita na tafiti nyingi imekamilika na unaanza utekelezaji wake (Mr Shotov) mradi huu utakuza uchumi wa taifa na kuelekea Tanzania ya neema huku ikiajiri watanzania Zaidi ya 1600.
Huu ni mmoja ya miradi inayotoa ahadi nzuri duniani kwa uranium safi na bora, mradi unaendeshwa na kampuni ya MANTRA ukizungumza Mkurungezi mkuu (Mr Frederick Kibodya)
Tunatakiwa kulinda rasilimali ya nchi hii kwa gharama yoyote kwa maslahi mapana ya maendeleo ya taifa na standard ni 50% kwa 50%.

Monday, October 16, 2017

OFA YA USHAURI WA KIBIASHARA KWA VIJANA 100 WAJASIRIAMALI

Tembea na Gecoso! 0788 275 331

Sehemu tano za ushari tunaotoa kwa watu 100.
1. Namna ya kutengeneza wazo nzuri ya kibiashara
2. Namna ya kuandika wazo hilo katika maandiko ya biashara
3. Namna  ya kurasimisha wazo lako la biashara
4. Namna ya kupata fedha za mtaji kutekeleza wazo lako
5. Namna ya kuanza biashara yako kwa mtaji mdogo sana
 

Sunday, October 15, 2017

SABABU 5 ZA KUANZA BIASHARA YAKO BILA MTAJI

KWA MSAADA WOWOTE TEMBEA NA GECOSO!


SAFARI YA MJASIRIAMAILI
Jenga Biashara yako kupitia unachokijua
Badala ya kuwekeza katika biashara kubwa kama kununua hisa au kampuni kubwa, hakikisha unajenga biashara yako katika ujuzi, kipaji na maarifa uliyonayo tayari. Kadri unavyo tegemea kidogo kutoka nje ndivyo unavyopata mafanikio makbuwa kupita biashara yako. Unapo fanikiw akujenga beashara yako kupitia ujuzi wako na unachokifahamu unapungiza msaada na ushari kutoka nje kuhusu maendeleo ya biashara yako. Alafu kuwa na ujuzi na maarifa yako ndicho kinafanya mafanikio yako katika safari yako ya ujasiriamali yenye tija.
Mwambie kilammoja kuhusu unachokifanya.
Kufahamisha familia yako, marafiki, mwasiliano ya biashara na hata uliosoma nao huko nyuma kuhusu biasara yako mpya ni mafanikio yako, maana hao ni mtaji. Piga simu, tuma email, na hakikisha biashara yako mpya inafahamika, pia weka kwenye mitando yako ya kijamii. Marafiki na wanafamilia watakusaidia kutangaza biashara yako na itafika mbali. Hii namna ya kutangaza baishara kuanzia chini itakufanya biashara yako ifahamike na kujulikana sana.
 Epuka gharama isiyo ya lazima.
Unaenda kuw ana gharama nyingi, na zingine haziepukiki kwa biashara yako. Kuepuka gharama isiyo ya lazima itakupunguzia matumizi mabaya ya fedha uliyo nayo. Tengeneza kitu kidogo kama kadi ya biashara yako ya gharama nafuu ili uwape wateja wako au marafiki.
Epuka kujizika na mikopo
Kuna njia nzuri sana yakutumia bila kujukua mikopo ya gharama kubwa, jifunze kutumia mikopo kama ya M-pawa, na timiza, au vikoba ili uepuke tozo kubwa ya kurejesha mkopo ambao utakuja kuzika biashara yako ndani yam da mfupi.  Kompyuta mpya, meza na viti vipya wa ofisi ni muhimu kuliko kuchukua vibovu na vikaharibika kwa wakati mmoja na umevipata kwa hela ya mkopo.Badala ya kununua kila kitu tumia hela ya biashara yako kununu vifaa vya ofisi na gharama za baishara yako kuliko hela nyngi kutoka mfukoni mwako. Epuka msongo wa mawazo kwa mikopo isiyo ya lazima, ili kupata fursa Zaidi ya kufanikiwa katika biashara yako.

Hakikisha madeni yako kwa watu hayakuangushi
Kama biashara yako ni ya rejareja basi hili halikuhusu, lakini kama unatoa hudma ya ushari wa kibiashara au bidhaa kwa watu wa biashara ndogondogo hikikisha unaweka sera nzuri ya malipo ya madeni yako kwa mda mfupi ili usikwame kufanya biashara. Usitengeneze sera ya malipo kwa kutafuta namna ya mkumfurahisha mteja wako ila isizidi siku 15 or 30 kupokea madeni yako nje.Weka sera katika misingi ya mafanikio yako siku zote.
Uwe tayari kuhaso ilikufanikiwa katika safari yako ya kijasiriamali.

Saturday, October 14, 2017

SAFARI YA MJASIRIAMALI,

Je, kwa nini hakuna mitaji kwa vijana wengi?
katika dunia tunayo ishi leo idadi ya vijana ni kubwa sana hasa katika nchi ya ulimwengu wa tatu na wa pili yaani nchi maskini na zile zenye uchumi unaokua kwa kasi. idadi hii kubwa ni nguvu kazi kwa maana ya rasilimali watu katika uzalishaji, uongozi na nyanja zote za maisha ya kawaida.

Vijana wetu wanakosa mitaji kwa kuwa hawana mambo makuu manne muhimu sana katika uchumi kama yafuatayo,
  1.   Ujuzi na usimamizi dhabiti wa rasilimali (yaani managerial competency) kijana anapokuwa na uelewa wakina juu ya mambo ya utawala wa rasilimali zilizopo utafanikiwa kupata fursa nyingi na kwa namna rahisi sana ili kuleta tija katika jamii anayoishi. Hii ina ambatana na ubunifu wa kujua ujuzi alionao kijana, kipaji, fursa watu iliyo mzunguka kama msemo usemao "maisha ni watu" watu ni wateja wa bidhaa na huduma mbalimbali.
  2.  Ujuzi na uwezo wa kapanga  mipango thabiti inayotekelezeka kwa uwezo wake mwenyewe (yaani proper planning and sustainable strategies). kijana wa karne hii lazima awe na uwezo mkubwa wa kuona mbali katika mawazo aliyonayo na kuyaweka kimkakati ili aweze kuleta maendeleo endelevu katika maisha ya kila siku na jamii yake. asipokuwa mbunifu katika mpangilio wa mipango yake itakuwa ngumu hata yeye kujua nini anahitaji kwa kiasi gani na lini kwa namna gani.
  3. Ujuzi na maarifa ya fedha (yaani financial intelligence) kijana akiwa na ujuzi mali na maarifa ya fedha ni rahisi kuelewa wapi anaweza kupata fedha bila kusahau mambo mengine hapo awali ilikupata pesa ya kuendesha miradi yake kwa mfano tanzania inatoa 5% ya mapato yake kuwezesha vijana has walio rasimisha miradi yako na wenye andika nzuri la miradi katika kila halmashauri nchini, kuna mashirika marafiki wa uchumi na maendeleo yanayotoa huduma pia. mtu mwenye ujuzi wa pesa halalamiki ugumu wa fedha ila unahitaji sera nzuri za uwekezaji na mazingira ya biashara na kulipata kodi stahiki.
  4. Mwisho ni Elimu na ujuzi wa uwekezaji (yaani Investment knowledge and skills) kijana mwenye kujua fursa na utaratibu wa uwekezaji ni rahisi kuamini uwezo wake wa kuleta mawazo yake kwenye mazingira ya uwekezaji kwa kufahamu fursa nyingi (incentive opportunities) katika baadhi ya sector na ushindini wa kimasoko katika mahali husika.

Saturday, October 7, 2017

Karibu kwenye blog ya gecoso media
Karibu sana kwenye blog ya Gecoso Media. Hii ni blog yako ya kukupa habari za kweli na uhakika. Tunakuahidi blog hii kuwa blog ya kwanza Tanzania kwa kutoa huduma nzuri za habari na mafunzo mbali mbali ya kukufundisha kuhusiana na maisha, ujasiriamali n.k.

Ukiwa na Tangazo unataka tukutangazie kwenye blog hii ni bei ndogo sana wasiliana nasi kwa haraka kupitia email hii gecosotz@gmail.com utajibiwa kwa haraka sana. Unachotakiwa ni kuelezea nini unataka kutangaza mfano kutangaza biashara, huduma au kutangaza blog au website ili ijulikane na watu wengi zaidi.


Vitu vizuri share na marafiki. watumie marafiki anwani ya blog hii ambayo ni gecosomedia.blogspot.com watumie kwenye magroup ya whatsapp facedbook na kwingineko ili nao waje kufaidika na habari zinazoandikwa kwenye blog hii ya kwanza kwa kutoa habari za kweli. Ukiwa na maoni comment hapa chini Karibu sana mdau